Jeshi
la vijana Watafuta Njia (PFC) wakionesha programu maalum katika sherehe
ya kumuaga Mch. Amosi Lutebekela (hayupo pichani) iliyofanyika katika
kanisa la waadventista wasabato Manzese jana.
Kwaya
ya wasabato ya Mbiu wakikabidhi zawadi ya kwaya kwa Mch. Amosi
Lutebekela na Mkewe kwenye sherehe ya kuwaaga iliyofanyika jana katika
kanisa la wasabato Manzese.
Kwaya
ya Wasabato Ruvu kitonga wakimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji wakati wa
sherehe ya kumuaga Mch. Amosi Lutebekela iliyoandaliwa na kanisa la
wasabato mtaa wa Manzese.
Kwaya
ya Angaza wakiimba wimbo maalum wa kumuaga Mch. Amosi Lutebekela kwenye
sherehe ya kumuaga iliyoandaliwa na kanisa la wasabato mtaa wa Manzese.
…………………………………….
Na. Sarah Reuben
Mkurugenzi
wa Sauti ya Unabii, Uchapaji na Maeneo Mapya Mch. Amosi Lutebekela jana
amekemea tabia mbaya ya baadhi ya waumini wa kanisa la waadventista
wasabato wanaoshindwa kutimiza kiapo chao cha ndoa na kuanza kudai
kuvunja ndoa kwa sababu zisizokubalika kibiblia.
Akizungumza
wakati wa ibada kuu katika kanisa la waadventista wasabato Manzese,
jijini Dar es Salaam, Mch. Lutebekela alisema hivi karibuni idadi ya
wanandoa ambao wanaomba kuvunja ndoa inaongezeka tena kwa sababu
zisizokubalika kibiblia.
“Mimi
kama msajili wa ndoa nimekuwa nikishughulikia changamoto mbalimbali za
wanandoa ambao wamekuwa wakiomba kuvunja ndoa kama suluhisho la migogoro
yao. Ninakemea wanandoa wote wenye malengo ya kuvunja ndoa kinyume na
utaratibu wa biblia. Tabia hiyo ikome mara moja kwa jina la Yesu,
alisisitiza.
Katika
hotuba yake vilevile Mch. Lutebekela aliwataka vijana ambao hawajaingia
katika ndoa kuzingatia sifa za kiroho zaidi badala ya kutegemea mivuto
ya kimwili yaani sura nzuri na muonekano wa nje. “Ninapenda kuwaasa
vijana wa kiume na wakike epukeni sana kutafuta wenzi wa maisha kwa
kuangalia mivuto ya nje yaani sura na muonekano. Sura inachakaa lakini
roho na tabia njema haitachakaa hata umri wenu ukisonga, alifafanua Mch.
Lutebekela.
Mch.
Amosi Lutebekela aliyasema hayo katika sherehe ya kumuaga rasmi
iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Manzese baada
ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Sauti ya Unabii, Uchapaji na Injili
katika maeneo mapya hivi karibuni. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi,
Mch. Lutebekela alikuwa mchungaji anayesimamia Mtaa wa Manzese.