Ajali
mbaya ya barabarani imetokea mkoani Tanga asubuhi hii wakati Basi la
Kampuni ya Simba Mtoto ya Tanga lilipogongana na Lori uso kwa uso katika
eneo la Pangamlima Wilayani Korogwe mkoani humo,taarifa za awali kutoka
eneo la tukieo zinaeleza kuwa watu 10 wanahofiwa kupoteza maisha na
wengine kujeruhiwa vibaya atika ajali hiyo.
Globu
ya Jamii bado inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu ili kupata
idadi kamili ya waliopoteza maisha.Mungu azilaze roho za marehemu mahali
pema peponi-AMIN