
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano
wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF
uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na
umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake wakati
akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa
siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika
hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa
PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii,
pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule
vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo
ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI -
MMG.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama
na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah
akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh.
Ashatu Kijaju.

Baadhi ya Wadau washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano
wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli
mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa
kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaji alipokuwa akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.