Kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),
Profesa Lawrence Museru akipokea msaada wa vifaa vya upasuaji na Dk
Julieth Magandi (wa pili kushoto) wakipokea msaada huo kutoka kwa meneja
wa shirika hilo, Bill Bali.
Kulia
ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja katika Hospitali
hiyo, Aminiel Aligaesha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa
Lawrence Museru wakifungua boksi lenye msaada wa vifaa vya upasuaji.
Vifaa vilivyotolewa leo na shirika hilo.
Picha zote na John Stephen- Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
HOSPITALI
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa vya upasuaji
vyenye thamani ya Dola 38,56.70 za Marekani ambavyo vimetolewa na
Shirika la kimataifa la misaada la Project Hope la Marekani.
Daktari
wa hospitali hiyo Julieth Magandi amesema kwamba vifaa hivyo vitatumika
katika shughuli ya upasuaji mbalimbali ukiwamo upasuaji wa macho na
mishipa ya damu.
Dk Magandi amelishukuru shirika hilo kwa kutoa msaada huo kwa kuwa utaongeza tija katika kazi za upasuaji kwenye hospitali hiyo.
“Tunaomba
msituchoke, tutakapohitaji msaada mwingine mtupokee ili Muhimbili
endelee kutoa huduma bora za afya kwa Watanzania,” amesema Dk Magandi.
Naye
Meneja wa shirika hilo nchini, Bill Bali amesema kwamba lengo lao ni
kutoa misaada mbalimbali ili hospitali hiyo itoe huduma bora za afya kwa
Watanzania.
Bali
amesema kwamba shirika hilo litaendeleza uhusiano kwa lengo la kuboresha
huduma za afya na kwamba wataendelea kutoa misaada katika maeneo mengi
ya hospitali hiyo.
Vifaa
hivyo vimepokelewa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo,
Profesa Lawrence Museru katika ukumbi wa mikutano wa hospitali hiyo.