
Meneja
Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akionyesha moja ya tangazo la ongezeko
la muda wa masaa ya vifurushi vya Airtel yatosha wakati wa kutangaza
muda mpya wa kuisha kwa vifurushi vya Airtel yatosha kwa siku kuwa ni
masaa 25. Yaani masaa 24 ya siku ongeza saa moja.
· Wateja wa Airtel waongezewa muda kufaidi zaidi katika vifurushi vya Airtel Yatosha
AIRTEL
Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yake ya kujali wateja wake kwa
kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel Yatosha hivyo kuvifanya
kuwa bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.
Akiongea
kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Aneth
Muga alisema "huduma yetu ya Airtel Yatosha inaendelea kukidhi mahitaji
ya Wateja wetu kwani vifurushi tunavyotoa sasa vya Airtel Yatosha vya
siku kwa shilingi 500 tumeongeza muda wake wa kutumika zaidi
ukilinganisha na vifurushi vingine vinavyotolewa sokoni
Bi.
Muga alisema sambamba na hili vifurushi vya Airtel Yatosha vinamuwezesha
mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote masaa
25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na 1 la
nyongeza.
Kikubwa
na kizuri zaidi bado pia mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata
nafasi ya kuingia kwenye droo ya promosheni yetu kabambe ya Airtel
Mkwanjika na kujishindia pesa taslimu hadi sh. Milioni moja"
Kujiunga
na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga
*149*99# na kisha kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel
yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi.