
Mkurugenzi wa
Mashtaka Nchini, (DPP), Bw. Biswalo Mganga, (katikati), akifafanua
jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ambao
ulimkutanisha yeye, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kutoka
jeshi la polisi, (DCI), Kamishna wa polisi, Diwani Athumani, (kushoto),
na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
(TAKUKURU), Bw.Alex Mfungo, kwenye makao makuu ya polisi jijiniDar es
Salaam, Januari 28, 2016. Katika taarifayao ya pamoja, taasisihizo
zimeanza kutaifisha mali za watuhumiwa wa Ufisadi na Uhujumu uchumi na
kuwataka wananchi kujitokeza kuwataja watuhumiwa wanaomiliki mali hizo
kokote waliko

Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga

DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo

Kamishna Diwani Athumani akizungumza


Waandishi wa habari wakiwa kazini

Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na watatu hao

Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akiuliza swali



Bw.
Oliver Stolpe, (kushoto) kutoka UNODC ambao ni wadau wa Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka DPP, akiwa na Mkuu wa Mahusiano Ofisi ya DPP, Bw.
Oswald Tibabyekonya wakitoka kwenye mkutano huo
.(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)