
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali
ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.
Kutokana na maombi ya
nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia
tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne tarehe mbili Februari 2016 ili
kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.
Pia TRA imeongeza
muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.
Waombaji wote wa
nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.
Tunaomba radhi kwa
usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.
Kwa maelezo zaidi
tafadhali wasiliana na:
kituo cha huduma kwa
wateja
08000780078,
0800750075, 0713800333
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na
Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu