Kassim Kayira, mtu ambaye hakuwahi
kuwaza kama angeweza kuwa mtu tajiri na maarufu kama alivyo, kupitia
uandishi wa habari na utangazaji, amepambana kujiweka mahali pazuri na
sasa anapata kila kitu alichokosa utotoni na anasimulia maisha yake.
Wiki iliyopita, aliishia pale alipoacha
kazi baada ya kuona mazingira siyo mazuri, kwamba aliundiwa zengwe baada
ya kuanika ufisadi mkubwa uliofanywa na viongozi katika serikali ya
Kagame, ikihusisha ununuzi wa magari ya kifahari.
Akaishia kueleza kuwa alikaa nyumbani
kwa muda wa siku tatu tu kabla ya kupata kazi nzuri yenye mshahara mara
mbili ya ule aliokuwa akilipwa hapo awali, Mungu alikuwa kazini.
SASA ENDELEA…
“Nilipata kazi kwenye shirika moja la
kutetea Haki za Binadamu la Inter News, nikawa nazunguka kwenye magereza
mbalimbali, mijini na vijijini kuzungumza na wafungwa, hususan
waliofungwa kwa kuonewa na ukiukwaji wa haki za binadamu,” anasema
Kayira.
“Kufikia hapo, umaarufu wangu ukazidi
kuchanua kila kukicha, sasa nikawa napokea maoni kutoka sehemu
mbalimbali za dunia, wakieleza jinsi walivyoguswa na kipindi hicho na
namna nilivyokuwa nikitangaza,” anasema.
“Warembo wa Rwanda nao hawakuwa nyuma,
ila kama nilivyosema hapo awali, mimi ni shehe, kwa hiyo imani yangu
ilinilinda sana, hawakuweza kupenya lakini tabu ikabaki kwa mke wangu,
hakuwa na amani kabisa na mazingira yangu ya umaarufu,” anasema Kayira
na kuachia tabasamu hafifu la kujilazimisha.
“Zaidi ya hapo, sasa nikawa
nimejietengenezea kundi kubwa la maadui, unajua kuna watu walifungwa kwa
sababu za kiuonevu, kisa mtu ana pesa au mamlaka, anataka amuonee mtu,
kwa hiyo nikawa navumbua uozo huo, watu wengi walirekebishiwa vifungo
vyao na hatimaye kuwa huru kabisa,” anasema Kayira.
“Nikawa naishi kwa tahadhari sana, sikuwa namuamini mtu,” anaongezea Kayira.
“Nikafanya kazi hadi mwaka 2003, nikawaza kuongeza elimu kwanza, hivyo mimi na familia yangu tukahamia nchini Uingereza, katika Chuo cha Greenwich, nikachukua Masters in Journalism lengo nikujiwekea wigo mkubwa wa kielimu,” anasema Kayira.
“Kwa hiyo elimu yangu si ya kawaida kidogo na sasa najipanga kuchukua PhD katika sheria,” anaongezea Kayira.

“Maisha yalikuwaje nchini Uingereza?,” namuuliza huku nikiwa makini sana.
“Tofauti ni kubwa sana kule, gharama za maisha ni kubwa, mfano katika chakula hali ni mbaya zaidi, unaweza kununua ndizi pakiti moja, kwa shilingi 20,000 za Kitanzania, maisha yakawa ya tofauti kidogo, lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea na mazingira hayo,” anasema Kayira.

“Nikasoma, lakini wakati naendelea na
masomo, nikakutana na aliyekuwa mhariri mkubwa sana kwenye Shirika la
BBC, upande wa redio akasema ananifahamu kwa hiyo alikuwa ananihitaji
sana kwa upande wa redio, nikakubaliana naye na kuanza kazi BBC, lakini
kwa upande wa Idara ya Kinyarwanda,” anasema Kayira.
“Idara ya Kinyarwanda? Sijaelewa kaka?” namuuliza nikitaka ufafanuzi zaidi.
“Yeah, kuna idara nyingi sana pale BBC, kuna idara inayohusika na Idhaa ya Kiswahili, Kifaransa, Kiingereza, Kinyarwanda na Kirundi, nilikaa zote hizo mbili kwa kuwa ni mtaalamu sana wa lugha hizo, nilizimudu kwelikweli,” anasema Kayira.

“Wakati naanza, yalikuwepo manyanyaso, dharau na kuonewa kutoka kwa mabosi wa humo ndani,” anasema Kayira.
“Mtu kwa kuwa tu ni mhariri au ana-
kicheo fulani anaamua kukuonea na kujiona yeye ni muhimu na bora zaidi,
lakini sikujali nikapiga kazi kama mwendawazimu, siku chache tu baadaye,
waliokuwa wakinionea, wakawa wanahitaji utaalamu kutoka kwangu na
hatimaye nikapandishwa cheo na kuwa bosi wao wote kwa kuwa nilikuwa na
uwezo,” anasema Kayira.
“Nikwambie kitu, mtu akikuonea, hususan
eneo la kazi, wala usijenge naye bifu au chuki, ulishawahi kuwaona kuku
nyakati za asubuhi wakiwa wanaenda kujitafutia riziki?” anasema Kayira
kwa mtindo wa swali.
“Yeah,” namjibu nikiwa na hamu kubwa ya kutaka kusikia alikusudia kusema nini.
“Kuku hutoka kwa mbwembwe na furaha kubwa sana, watakaa huko kutwa nzima wakitafuta chakula lakini ikifika jioni, lazima kuku hao warejee bandani,” anasema Kayira na kunitazama usoni huku akisikilizia kama nitamuuliza jambo. Hakuwa amekosea, ikabidi kuuliza.
“Unamaanisha nini kwa msemo huo kaka?” namuuliza huku nikijitengeneza vyema kwenye kiti kusikiliza maana halisi ya mfano wake.“Kuku hutoka kwa mbwembwe na furaha kubwa sana, watakaa huko kutwa nzima wakitafuta chakula lakini ikifika jioni, lazima kuku hao warejee bandani,” anasema Kayira na kunitazama usoni huku akisikilizia kama nitamuuliza jambo. Hakuwa amekosea, ikabidi kuuliza.
Unataka kujua alimaanisha nini? Usikose kufuatilia wiki ijayo