Stori: Mayasa Mariwata na Brighton Masalu
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameifuta aibu ya familia iliyokuwa ikiwakabili kwa kuamua kuifanyia ukarabati nyumba aliyozaliwa na kukulia, iliyopo maeneo ya Tandale-Uzuri jijini Dar Risasi linaripoti.
MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameifuta aibu ya familia iliyokuwa ikiwakabili kwa kuamua kuifanyia ukarabati nyumba aliyozaliwa na kukulia, iliyopo maeneo ya Tandale-Uzuri jijini Dar Risasi linaripoti.
Novemba 2, mwaka huu, gazeti la Ijumaa
Wikienda liliripoti habari ilionesha kuwa nyumba hiyo ambayo anaishi
mama’ke mdogo Diamond na ndugu wengine, inamtia aibu yeye na familia
nzima kwani choo chake kimeharibika na kimejaa hivyo kuleta usumbufu kwa
majirani.
Mtoa ‘ubuyu’ mmoja wa kujitegemea
aliwaambia waandishi wetu kuwa baada ya gazeti hilo kuripoti habari
hiyo, Diamond alijisikia vibaya akaamua kumpa jukumu la ujenzi mama yake
mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ aende kusimamia ujenzi huo.
“Njoeni
Tandale mtamkuta mama D (mama Diamond) yupo bize kwelikweli kusimamia
ujenzi wa nyumba ile iliyokuwa inatia aibu, ameongeza kozi mbili juu,
anaweka paa la Mzauz, yani ikikamilika itakuwa bomba balaa,” alisema
mtoa ubuyu huyo.
“Mnataka kusema nini? Maana Nasibu (Diamond) ameamua kukumbuka kwao kwa kukarabati, amezaliwa na kukulia hapa, hii ni nyumba ya bibi yake, na chumba alichokuwa akiishi Diamond kipindi hicho ni hiki,” alisema mama Diamond huku akiwaelekeza waandishi wetu kwa ufasaha chumba hicho