
Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza na
waandishi wa habari jinini Dar es Salaam leo wakati wa kuwapokea
wanafunzi kumi kutoka vyuo mbalimbali ili kwenda kuwapa mafunzo na
kufanya kazi katika benki hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa rasiliamali
fedha wa kampuni ya Deloitte Paul Mbithi na kushoto ni Mkuu wa kitengo
cha utumishi wa Benki ya Barclays Tanzania, Eutropia Mwabeleko.

Mkuu
wa kitengo cha utumishi wa Benki ya Barclays Tanzania, Eutropia
Mwabeleko akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
wakati wa kuwapokea wanafunzi kumi kutoka vyuo mbalimbli hapa nchini
kwaajili ya kwenda kuwapa mafunzo ya kufanya kazi katika benki hiyo.

Mmoja
wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Neema Munuo akiushukuru
uongozi wa benki ya Barclays kwa kuwachagua kwenda kufanya kazi katika
benki hiyo.

Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina katikati waliokaa
akiwa na wanafunzi wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini wakiwa
katika picha ya pamoja leo jijini Dar es Salaam.