Kutuma pesa Airtel kwenda Airtel bila
kikomo Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua ofa kabambe
itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa marafiki na
familia zao ndani ya mtandao wa Airtel Bure Ofa hii mpya ijulikanayo
kama "Okoa Mapene'' ina lengo la kuinua huduma za kifedha na kuwapatia
wateja njia rahisi ya kufanya miamala yao ya kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson
Mmbando alisema " kwa mara nyingine tena tunadhirisha kwa vitendo
dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu, rahisi na zenye gharama nafuu
kupitia huduma ya Airtel Money. Leo tunawawezesha wateja wetu wa Airtel
money nchi nzima kuokoa pesa wanapotuma pesa kwenda kwa mtumiaji wa
Airtel kwani tozo za kutuma pesa ni BURE kwa kiasi chochote
kitakachotumwa. Tunaamini ofa hii ya "Okoa Mapene'' itakuwa kichocheo
kikubwa kwa wateja kutumia huduma ya Airtel Money kwa muda wa mienzi
mitatu na zaidi"Aliongea kwa kusema "Okoa Mapene'' ni njia mojawapo ya kuwazawadia wateja wetu wanaotuma pesa kwa ndugu , jamaa, marafiki, familia na washirika wao wa biashara kupitia huduma ya Airtel Money. "Okoa Mapene'' pia kuwawezesha mawakala kupata kamisheni zaidi kutokana na kuwa na wateja wengi watakaofanya miamala mingi kuanzia sasa.
Ili kupata kutuma pesa mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Money na kuanza kufanya miamala yake BURE.Hiv karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawiwo la faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea gawiwo hilo moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu.