Mkongwe wa muziki kutoka Naija na mkurugenzi wa Lebo ya Muziki ya MAvin, Don Jazzy.
MKONGWE wa muziki kutoka Naija na mkurugenzi wa Lebo
ya Muziki ya MAvin, Don Jazzy anatarajia kuja na tamasha bab’ kubwa la
kusherehekea lebo yake, Desemba 23, mwaka huu.

Akizungumza
na vyombo vya habari Nigeria, Don Jazzy alisema wameamua kuandaa
tamasha hilo kama shukurani kwa mashabiki wao ambao wamekuwa
wakiwaonyesha sapoti tangu mwaka 2012 ilipoanza kujipatia umaarufu
zaidi.
“Mipango ya tamasha letu inakwenda vizuri, nachukua nafasi hii
kuwashukuru wadhamini wetu wakuu ambao ni Benki ya Access na mashabiki
wetu waliotuunga mkono tangu mwaka 2012,” alisema Don Jazzy.
Mavin Records ina vichwa kibao ambavyo vinabamba kunako muziki wa
Nigeria na Afrika kwa ujumla ambavyo ni Tiwa Savage, Reekado Banks na
Korede Bello.