

Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WANACHAMA
wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa
baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao.
Mbali
na hilo, waajiri wa metakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao, kujiunga
na mfuko wasio upenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza.Kauli hiyo,
ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa
Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa
elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.
Mkurugenzi
wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA,
Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai
kuwa haiwezi kufa.Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa
Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai
stahiki zao badala ya kulalamika.