Oct 12, 2015

RAIS DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WAMA SHARAF HUKO LINDI


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndugu Yahaya Nawanda baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi Mjini kwenye sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo tarehe 11.10.2015.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Bwana Ibrahim Sharaf, Rais wa Sharaf Group of Companies ya nchini Dubai mara baada ya kuwasili kwenye Shule ya Sekonadi ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi. Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya uzinduzi wa Shule hiyo tarehe 11.10.2015.


 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiondoa kitambaa kwa kushirikiana na Bwana Ibrahim Sharaf aliyefadhili ujenzi wa Shule ya Wasichana ya WAMA Sharaf ikiwa ni ishara ya kuizindua rasmi. Baadaye Rais Dkt. Kikwete akishirikiana na viongozi wengine walisaidia ujenzi wa shule hiyo kukata utepe ikiwa ni mwendelezo wa sherehe za ufunguzi rasmi wa shule hiyo huko Lindi tarehe 11.10.2015.