
Afisa
Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi
Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey-Wanawake – Kidawa Abdallah (watatu
kushoto) leo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo NMB ilitangaza
udhamini wake kwa Timu ya Taifa ya Hockey inayotarajiwa kushiriki
mashindano ya Afrika kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki (Olympic
Qualifier) mashindano yatakayoanza Oktoba 23 mwaka huu. Wakishuhudia
kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo –
Juliana Soda na Kocha wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina
Quaranta (kulia).

Afisa
Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi
Kapteni wa Timu ya Taifa ya Hockey-Wanaume – Amarjeet Ruprai.

Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Yasoda (Wapili
kushoto) akikabidhi bendera ya taifa kwa Kapteni wa Timu ya Taifa ya
Hockey

Kocha
wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina Quaranta (kulia)
akitoa shukurani kwa NMB kwa niaba ya Timu ya Taifa ya Hockey.
NMB YADHAMIRIA KUINUA WANAWAKE KUPITIA MICHEZO
NMB YADHAMIRIA KUINUA WANAWAKE KUPITIA MICHEZO
Benki
ya NMB imeidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey katika mashindano
ya Africa Olympic Qualifier yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23, 2015
mpaka Novemba 1, 2015 – Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa na lengo la
kuinua maisha ya wanawake kupitia michezo.
Udhamini
huo ni pamoja na kutoa tiketi za ndege kwa wachezaji wote na viongozi
pamoja na vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mavazi ya safari kwenda
Afrika ya Kusini vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 17.
Afisa
wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema benki ya NMB marazote
hufarijika inapopata nafasi ya kusaidia michezo kwani kwa kufanya hivyo
inaonyesha kujali kwao kwani miongoni mwa wapenda michezo na wachezaji
wenyewe, ni wateja wa NMB.
“Tunaamini
michezo ni muhimu katika kubadilisha maisha ya wachezaji ambao wengi
wao ni vijana, hivyo udhamini wetu kwa Timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey
Tanzania utaongeza chachu ya ushindi kwa mchezo ambao unaonekana mgeni
Tanzania, tunaamini mchezo huu pia utatoa fursa kwa vijana kupata ajira
pamoja na kuitangaza nchi yetu kupitia michezo ya Olimpiki.” Alisema
Bwana Barnabas