Queen wa ngoma ya 'Hakunaga' maarufu kwa jina la Lady Queen
ambaye ni mwanadada mwenye umri wa miaka 23, 'Makelele na wewe' pia ni Track
yake ambayo aliwahikufanya na Dullayo.
Hapa ni wakati alipo fanikiwa kukutana
na mwandishi wetu face to face ambapo mwandishi wetu alimtaka Lady Queen
kuzungumzia Tasnia ya muziki wa hapa bongo kufuatia yeye ni mdau ambaye
anategemea hapo baadaye aje kuishi maisha mazuri kupitia sanaa ya muziki. Baada
ya msanii huyo ambaye anachipkia kwa kasi nzuri kupata fursa ya kufafanua
muziki hiki hapa chini ndicho alicho zungumza.
LADY QUEEN: "Muziki wa Bongo fleva kiukweli umekuwa na
ushindani mkubwa maana kila mmoja anatamani kufika mbali na kuwa juu ya mwenzie
kwa kufanya vitu vizuri, so sasa hivi tunaangalia wakubwa zetu walifanya nini
yaani ambao tayari muziki wao wameufikisha mbali mfano kama Vanessa, so nasisi
tunaiga njia walizo tumia ili tuweze kufikisha na sisi muziki wetu
panapotakiwa, kwa hatua hiyo naona tunaelekea pazuri kimuziki."
LADY QUEEN: " Naangalia kitu ambacho nikiimba kila mmoja
atatamani kusikiliza watoto kwa wakubwa haijalishi ni wimbo wa mapenzi au laa!
pia now nipokwenye mchakato wa kuboresha kucheza coz nafanya mazoezi ya kudance
maana hata nikiwaga kwenye stage huwa natamani nicheze vizuri ili mashabiki
wangu wa -Enjoy".
LADY QUEEN: "Kwenye muziki kiukweli ugumua ambao nauona ni kwenye kupata connection, maana hadi wadau wa muziki wakufahamu inahitajika juhudi ya kutosha, katika muziki wangu kitu ambacho naona kinamiss ni ushirikiano, maana baadhi ya mastaa wanatutenga sisi upcoming Artist unakuta mastaa kwa mastaa ndio wanakuwa na ushirikiano, so inakuwa ni ngumu kwetu kuyafikia malengo, mimi huwa najitahidi kuonesha ushirikiano kwa wasanii wote hasa kwa kuposta kazi zao ili basi hata namimi ninapo toa kazi zangu waweze kunisuport hata kwa kushare kazi ambayo nakuwa nimeitoa hiyo ni moja ya jitihada zangu."

LADY QUEEN: "Natamani sana kufikia level ya Vanessa Mdee na
hata katika ndoto zangu ni kujakufanyanaye kazi, so kwa sasa najitahidi
kutengeneza mazingira mazuri kwa kutoa kazi nzuri ili hata siku nikisema
nimfuate kusiwe na ugumu wa yeye kukubali kufanya kazi na mimi I wish.
Sitegemei kutoka kwa kukutumia skendo za kutengeneza maana nikitu ambacho
nakishangaa sana coz unakuta msanii ni maarufu halafu anatengeneza skendo huko
nikujishusha, nafuu sikendo ya kweli kuliko ya kufoji huo ni ushauri wangu kwa
wasanii wanaopenda skendo."
LADY QUEEN: "Mwisho napenda kuwaambia mashabiki wangu kuwa
nashukuru 'Hakunaga' wameipokea vizuri kinacho fuata ni zaidi ya 'Hakunaga'
baada ya uchaguzi nitaachia Audio & Video ya wimbo wangu mpya ambao unaitwa
'Chunga Mzigo wako'. Stay tuned nawapenda sana."
link ya clip yake here: https://www.youtube.com/ watch?v=ZAA8qctgdMI&feature= share