Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Profesa Adolf Mkenda ( wa pili kushoto )
akimkabidhi cheti Msafiri Mpendu muda mfupi mara baada ya kufunga ya
siku tatu yaliyolenga kujenga uelewa juu ya mpango wa serikali wa
kushirikisha sekta binafsi kushiriki katika miradi mikubwa kupitia ubia
kati ya sekta ya umma na binafsi (kushoto ) ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini Godfrey Simbeye, ( wa tatu kushoto ) ni
Kamishna wa PPP Frank Mhilu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Bw.Godfrey Simbeye
akisisitiza jambo kwenye mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa
wajasiriamali wakubwa na wakati juu ya mpango wa serikali wa
kushirikisha sekta binafsi kushiriki katika miradi mikubwa kupitia ubia
kati ya sekta ya umma na binafsi ( PPP) mafunzo hayo yaliyoandaliwa na
Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki ya Dunia yalifungwa jijini Dar
es Salaam.