Oct 10, 2015

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UMEPIGA HATUWA KUBWA

Mkurugenzi wa Matibabu na Huduma za kiufundi Dr. Frank Lekey akizugumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya miaka kumi ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania,Dokta Jakaya Kikwete, Mfuko umepiga hatua kubwa ya maendeleo, idadi ya wanachama wachangiaji 640,341 na idadi ya wanufaika ni 3,237,434 kikao hicho kimefanyika leo jiji Dar es Salaam
 Waandishi wa habari wa kimsikiliza  Mkurugenzi wa Matibabu na Huduma za kiufundi Dr. Frank Lekey kikao hicho kimefanyika leo jiji Dar es Salaam
 
 
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni Taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria Namba 8 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1999, ikiwa na jukumu la kusimamia huduma za matibabu kwa wanachama na wategemezi wao kupitia vituo vya ngazi mbalimbali za matibabu ( zahanati, vituo vya afya, hospitali na maduka ya dawa).  Mfuko ulioanza kutoa rasmi huduma kwa wanachama wake Mwezi Oktoba, 2001. 

        Katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dokta Jakaya Kikwete, Mfuko umepiga hatua kubwa ya maendeleo kama inavyoelezwa hapa chini:
       Takwimu za mafanikio katika kipindi cha miaka kumi (2005 hadi 2015) katika maeneo mbalimbali ni kama ifuatavyo:
Usajili wa Wanachama wa NHIF na CHF.
A: Wanachama wa NHIF
SN
MWAKA        2005
MWAKA         2015
Ongezeko la Asilimia
1
Idadi ya wanachama Wachangiaji 275,865
Idadi ya Wanachama Wachangiaji  640,341
132
2
Idadi ya Wanufaika 1,268,979
Idadi ya Wanufaika  3,237,434 
155


B: Wanachama wa CHF:
SN
MWAKA        2009
MWAKA         2015
Ongezeko la Asilimia
1
Halmashauri zilizotekeleza  99
Halmashauri zinazotekeleza  144
87%
2
Idadi ya Kaya 120,000
Idadi ya Kaya 1,112,874

927%
3
Idadi ya Wanufaika 720,000
Idadi ya Wanufaika  6,677,244
927%

Hivyo hadi kufikia Juni 2015 jumla ya wanufaika wa NHIF na CHF ni 9,914,678 ambayo ni sawa na asilimia 22.8 ya Watanznaia wote kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

Jukumu lingine la NHIF ni kusajili vituo vya matibabu ambapo wanachama na wategemezi wao wanakwenda kupata huduma, katika kipindi cha miaka kumi, takwimu za usajili ni kama ifuatavyo:
Maelezo
2005/06
2011/12
2012/13
2013/14
2014/15
Zahanati
3,346
4,240
4,513
4,621
4,744
Vituo vya Afya
385
549
591
605

614
Hospitali
200
234
238
246
254
Maduka ya Dawa
36
143
169
178
202
Maduka ya Dawa Muhimu
 -
260
326
358

361
Kliniki za Vipimo
-
-
2
3

8
Vituo vya Uchunguzi
-
-
1
1

2
Jumla
3,967
5,426
5,840
6012
6,185

Malipo kwa Watoa Huduma:
Jukumu lingine la NHIF ni kuwalipa watoa huduma, ambapo tangu mwaka 2005 hadi kufikia Juni 30, 2015, jumla ya Shilingi Bilioni 555,008.80 zimelipwa kwa watoa huduma. (Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Vituo vya Uchunguzi na maduka ya dawa).

Mahudhurio katika vituo vya matibabu:
Katika kipindi cha miaka kumi cha kuanzia 2005 hadi 2015 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umelipia mahudhurio 27, 394,173 ya matibabu ya wanachama na wategemezi wao katika vituo vilivyosajiliwa.
Mikopo ya Ukarabati, vifaa tiba, TEHAMA na dawa:
Ili kuboresha huduma Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulianza kutoa mikopo ya ukarabati wa majengo, vifaa tiba, TEHAMA na dawa tangu mwaka 2007.


Katika kipindi cha miaka nane tangu mwaka 2007 hadi 2015 mikipo iliyotolewa ni kama ifuatavyo:
SN
AINA YA MIKOPO
IDADI YA VITUO
JUMLA YA FEDHA
1

Ununuzi wa Vifaa  Tiba
162
6.912 Bilioni
2

Ukarabati wa Majengo
36
4.120 Bilioni


Jumla
198
11.032 Bilioni

Miradi ya Uboreshaji wa Huduma za Matibabu:
Serikali ya Awamu ya Nne kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanza ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Matibabu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Kituo cha Mfano cha Matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Dodoma na majengo pacha katika Taasisi ya Tiba za Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI). Matarajio ya Serikali ya Awamu ya Nne ni kwamba miradi hii itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto mbalimbali zinazoikakabili sekta ya Afya nchini.

Huduma za Madaktari Bingwa.
Tangu mwaka 2012 Mfuko umeanza mpango kabambe wa kuwapeleka MADAKTARI  BINGWA katika maeneo ya pembezoni mwa nchi yetu kwa ajili ya kutoa huduma maalumu. Hadi kufikia Juni 30, 2015 Mfuko umetoa huduma hizo katika mikoa ya Lindi, Kigoma, Pwani, Rukwa, Katavi, Manyara, Tabora, Mtwara, Shinyanga, Simiyu na Mara ambapo zaidi ya wananchi 9,232 walihudumiwa katika maeneo hayo na zaidi ya wananchi 370 walifanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali katika mikoa iliyotembelewa.

Madaktari bingwa walioshiriki katika zoezi hili walitoka katika Hospitali ya Taifa wa Muhimbili, Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Madaktari hao ni mabingwa wa magonjwa ya moyo, magonjwa ya wanawake, magonjwa ya watoto, magonjwa ya ndani, magonjwa ya figo, wataalamu wa upasuaji na dawa za usingizi na huduma za wagonjwa mahututi.

KAULI MBIU YETU: HUDUMA BORA ZA MATIBABU NI HAKI YAKO NI DHAMANA YETU.