
Naibu
mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso akiongea na waandishi wa
habari leo hii katika ukumbi wa Hyatt Regency juu ya maandalizi ya
Rotary Dar Marathon 2015 ambayo huandaliwa na Rotary klabu za Dar es
salaam kwa kushirikiana na Benki M. Mbio na matembezi ya Dar Rotary
Marathon kwa mwaka huu zitafanyika katika viwanja vya Green, Oysterbay
tarehe 14 October 2015. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Rotary
Bi. Sharmila Bhatt, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi. Agnes
Batengas, Makamu wa Raisi wa Rotary klabu Oysterbay Bi. Anne Saels na
Rais wa Rotary Klabu Dar North Bw. Masato Wassira.

baadhi
ya washiriki wa Rotary Dar Marathon kutoka Malawi na Kenya wakifuatilia
mkutano huo, Marathon ya mwaka huu itajumuisha wakimbiaji kutoka nchi
za Kenya, Rwanda, Malawi, South Africa na Ethiopia.
Mbio
na matembezi ya hisani za Dar rotary marathon yanatarajiwa kufanyika
siku ya jumatano tarehe 14.10.2015 hapa jijini Dar es salaam ambapo
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais mstaafu mheshimiwa Ally Hassan
Mwinyi.
Mbio
na matembezi hayo yameandaliwa na klabu sita za Rotary za hapa Dar es
salaam kwa kushirikiana na Benki M na kauli mbiu ya mwaka huu ni
“kuponya maisha, badilisha jamii” ambapo fedha zitakazochangishwa
ziltaelekezwa katika ujenzi wa kituo cha afya hapa Dar es salaam.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI