

Nahodha Msaidizi wa Timu ya Mpira wa
Pete wa Idara ya Uhamiaji,Juliana Mwakalemela
akimkabidhi Kikombe cha Ushindi katika Michuano ya Klabu bingwa wa mpira
wa pete Tanzania,Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji,Piniel
Mgonja katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini
Dar es Salaam.

Wanamichezo wa mpira wa pete wa idara
ya uhamiaji wakisherekea kombe baada ya kufika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji
leo jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo wakimsikiliza Kamishina
wa Utawala na Fedha wa Idara ya
Uhamiaji,Piniel Mgonja (hayupo pichani) leo baada kukabidhi Kikombe cha Ushindi
katika Michuano ya Klabu bingwa wa mpira wa pete Tanzania leo Makao Makuu ya
Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TIMU ya Mpira wa Pete ya Idara ya
Uhamiaji,imeibuka mshindi katika michuano ya mashindano ya Klabu bingwa wa
mpira wa pete baada ya kuipiga timu ya Mbweni JKT iliyokuwa ikishikilia ubingwa
huo.
Akizungumza baada ya kupokea kombe
hilo ,Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idra ya Uhamiaji,Piniel Mgonja amewataka wachezaji wa timu hiyo kujituma na
kuweza kulinda kombe hilo ililisichukuliwe katika michuano mingine.
Mgonja amesema katika mwaka huu
wamekuwa wakishinda katika masuala mbalilmbali hivyo kushinda huko inatokana na wafanyakazi
kujituma kuaniza kutoa huduma hadi michezo.
Aidha amewataka wafanyakazi kuonyesha
vipaji vyao katika michezo mbalilmbali ili kuweza kufanya vizuri katika michezo
na kuweza idara ya uhamiaji kuwa ni
sehemu ya vipaji.
Nahodha wa timu hiyo wa Idara ya
Uhamiaji,Nina Muliga ameitaka Idara kuwawezesha kuanzia viwanja pamoja na
rasilimali fedha ili kuongeza ufanisi wa michezo mbalimbali wa kuleta ushindi.