Meneja
wa Wateja Binafsi wa First National Bank, Francois Botha na Meneja wa
Usambazaji na Matawi wa benki hiyo wakizindua mpango maalum
unaohamasisha Watanzania kujiwekea akiba na kujiwekea mustakabali salama
kifedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam leo Oktoba 1,
2015.
BENKI
ya FNB Tanzania imetoa wito kwa Watanzania kujijengea mustakabali
salama kifedha kwa kuendelea kuweka akiba zaidi benki kupitia fursa ya
mpango mpya wa benki hiyo wa “Weka akiba na ushinde”.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois
Botha wakati akizindua mpango huo jijini Dar es salaam ambapo alisistiza
umuhimu wa kuweka akiba. Mpango huo wa Weka Akiba na Ushinde utaanza
tarehe 1 Oktoba na kuendelea mpaka mwisho wa Disemba 2015.
Ikiwa
ni sehemu ya mpango huo utakaodumu kwa miezi mitatu, wateja waliopo na
wateja wapya wataingizwa moja kwa kwenye droo kutokana na akiba ya kila
shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao, kwahiyo watakaoweka
akiba zaidi watapata nafasi ya kushinda shilingi milioni 5 ambazo
zitatolewa kila mwezi kwa kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo iko wazi
kwa watu wote kushiriki.
Botha
alisema, “Katika kuendeleza utamaduni wa benki hii kuwatunuku na
kuwanufaisha wateja wake huku ikiendelea kutoa huduma za kisasa za
kibenki, FNB inatoa fursa hii kwa wateja kuweza kujinufaisha kutokana na
kuweka akiba huku wakijijengea mustakabali salama kifedha”.
chanzo ; JIACHIE