Oct 10, 2015

BUZWAGI YAWAZAWADIA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA.

Meneja wa Idara ya Maboresho ya Biashara wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Richard Ojendo wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja wa mgodi, “General Manager Prestegious award” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) anaeshuhudia upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyekuwa Shinyanga.
Meneja wa Idara ya Maboresho ya Biashara wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Richard Ojendo wa kwanza kushoto, mkuu wa wilaya ya Kahama bwana Benson Mpesya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja na Bwana Ojendo mara baada ya kutunukiwa uzo ya  akipokea tuzo ya heshima ya utumishi uliotukuka ya meneja wa mgodi, “General Manager Prestegious award”.
Meneja wa Idara ya Madini wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Muganda Mutereko wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) anaeshuhudia upande wa kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi.
Meneja wa Idara ya Ufanisi wa Kampuni wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga wa kwanza kushoto akipokea tuzo ya ya mshindi wa pili kwa nafasi ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya,(katikati) kulia ni Eng. Philbert Rweyemamu.
Mkuu wa kitengo cha Uchenjuaji wa Dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Festo akimpokelea Tuzo ya Mshindi wa tatu Bwana Karel Schultz ambaye ni meneja wa Kinu cha Uchenjuaji wa Mgodi wa Buzwagi mara baada ya kutangazwa mshindi wa tatu katika nafasi ya Meneja Bora wa Mwaka ”Best Manager of the year” tuzo hiyo ilikabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya.
Washindi wa Tuzo ya Meneja bora wa mwaka wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi.(kutoka kushoto ni Saimon Sanga Meneja wa Idara ya Ufanisi, wa pili ni Eng. Muganda Mutereko Meneja wa Madini, wa tatu ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Benson Mpesya na wa nne ni Eng.Philbert Rweyemamu aliesimama upande wa kulia ni bwana Festo aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya bwana Karel Schultez