BOXING: KUMBUKUMBU YA MUHAMMAD ALI NA MZEE CHOKA NDANI YA DAR ES SALAAM
Ali akiwa ana spar na Esmail Choka (Marehemu)
(Source: Midladjy Maez)
Boxer mashuhuri sana duniani Muhammad Ali waliwahi
kuja nchini kwetu mwaka 1980...Kilichomleta Ali ni kitu kimoja nacho ni
kutaka nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania kutojihusisha na Olympics ya
Moscow kutokana na Urusi kuihodhi Afganistan...Ali alivyokuja Dar
alipolekewa vizuri na Esmail Manambi Choka (Marehemu) na watu
wengi...Picha hapo juu ilichukuliwa Dar International Airport sasa ni
JNIA inaonyesha jinsi gani mzee Choka alivyo kuwa mshabiki mkubwa sana
wa Ali...Hapo chini kuna clip ya Ali alivyokutana na wadau Dar...