Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),
Mussa Jallow (wa tatu kushoto), akikabidhi pikipiki kwa Mwenyekiti wa
Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani, katika hafla ambayo
NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni
sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kuisaidia jamii. Hafla ya
makabidhiano ilifanyika Kibaha, Pwani jana. Wengine ni baadhi ya
wanachama wa TAS na maofisa wa NBC.
Meneja
wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa tatu kushoto)
akikabidhi pikipiki kwa mmoja wawakilishi wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa
wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki
tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za
benki hiyo katika kuisaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika
Kibaha, Pwani jana. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC,
Alina Maria Kimaryo na Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani.
Meneja
Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara( NBC) Alina Maria Kimaryo
(kushoto), akizungumza na baadhi ya wanachama wa Chama cha Albino (TAS)
Mkoa wa Pwani katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia,
miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo
katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao.
Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha mkoani Pwani jana.