Baadhi ya
waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali nchini wakiwa kwenye hafla
fupi ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni
4.9 kwa timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom
Tanzania bara (VPL) leo vilivyokabidhiwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo
kampuni ya Vodacom Tanzania.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi kuu ya mpira wa miguu Tanzania
bara leo imekabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vyenye
thamani ya shilingi milioni 490,000,000/=
Akikabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es
Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin
Twissa,alisema kuwa kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya
soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi vifaa mbalimbali vya ligi
ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda
ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi
vinavyohitajika.
“Tunajisikia furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi wa 2015/2016”Alisema Twissa.

Twissa alisema Vodacom inaendelea
kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa
nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao
baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya mchezo waupendao pia
siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote,ikiendelezwa
inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato
makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Aliwataka wadhamini wengine kujitokeza ili
kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na kuongeza maslahi kwa wachezaji
wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha nguvu timu zetu zinaweza kuwa na
wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu kwa wadau mbalimbali kuanza
kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa kuwa vipaji vinaanzia ngazi
ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na kuendelezwa ”Alisema Twissa.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya
Ligi,Boniface Wambura aliishukuru Kampuni ya Vodacom, na kuvitaka
vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini
wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.
Aliongeza kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika mapema pia timu zitazoshiriki zimeziandaa vya kutosha kuhakikisha ligi inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.