Sep 2, 2015

AIRTEL YAZINDUA OFFA KABAMBE YA SMARTFONIKA KWA WATEJA WAKE

Meneja Uhusiano wa Airtel , Bwana Jackson Mmbando (Kulia) akimuonyesha Afisa Mauzo wa Airtel   Michael Nasare  simu aina ya Samsung J100 iliyo na Selfie Stick ya kupigia picha, wakati wa uzinduzi wa offa  ijulikanayo kama “Smartfonika Ujiselfonishe” inayowawezesha wateja kupata simu mbalimbali za kisasa pamoja na kifurushi cha internet,sms na muda wa maongezi bure.


Airtel Tanzania, mtandao wa smartphone kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung leo imezindua offa kabambe ijulikanayo kama “smartphonika na ujiselfishe na Samsung J100” itakayowapatia wateja wake simu mbalimbali za kisasa za smartphone.
Akiongea kuhusu ofa hii , Meneja Uhusiano wa Airtel , Bwana Jackson Mmbado alisema “Hii ni moja kati ya ofa nyingi ambazo Airtel imetoa kwa wateja wake kwa lengo la kuwawezesha kwenda sambamba na techonologia mpya na simu za kisasa.
Simu hii aina ya Samsung J100 ilizinduliwa na kuletwa sokoni mwanzo mwa mwaka huu, ni simu bomba inayokuja na selfie stick itakayowaweesha wateja wetu kuchukua matumio muhimu na wapendwa wao kwa kupiga picha za selfie zenye ubora wa kipekee katika ulimwengu huu wa selfie , vilevile camera ya simu hii aina ya 5 MP, 2592 х 1944 pixels, autofocus, LED flash inatoa picha zenye ubora ambazo mteja ataweza kuzituma kwa marafiki na jamii kupitia mitandao ya kijamii.
Samsaung J100 ina ukubwa wa memory card yenye ukubwa wa 8GB pamoja na simu yenyewe ina ukubwa wa 4GB itakayowawezesha kuhifadhi kumbukumbu muhimu kama vile mafile na picha, betri ya simu inadumu kwa muda wa masaa 10 na kumwezesha mteja kutumia simu yake siku nzima bila kuwa na kifaa kingine cha kusaidia simu itakapozima kama vile powerbank. Samsung J100 inakuja kwa rangi tofauti ikiwemo rangi nyeupe, nyeusi na Bluu na kumpa mteja uhuru wa kuchagua rangi anayoipenda ”.
“ Tumefanya hivi kwa vile tunawajali wateja wetu na tunataka waende sambamba na mabadiliko ya technologia huku tukiwawezesha kupata huduma bora na nafuu za mawasiliano. mteja yoyote atakayenunua simu aina ya Samsung J100 katika duka lolote la Airtel nchini nzima inayouzwa kwa shilingi 230,000/= hapo hapo atapata ofa ya kifurushi cha internet cha 2.4GB, ujumbe mfupi wa 2400, na dakika 2400 za maongezi, vifurushi hivi vinaweza kutumika kwa muda wa mwaka mzima Bure.”Aliongea Mmbando.
Wateja wa Airtel Tanzania sasa wamehakikishiwa huduma na bidhaa za kibunifu kupita mtandao wa mawasiliano ulionea zaidi nchini na kuwafikia zaidi ya asilimia 85 ya wakazi katika miji na vijiji mbalimbali nchi nzima.