Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa, Sifuni Mchome
akizungumza wakati wa makubaliano ya mkataba wa mkopo kati ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA, Joel Laurent na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TIE,Dk.Paul Mushi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome
akisaini makubaliano ya mkataba wa mkopo kati ya Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA) Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) iliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam,Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TEA,Joel Laurent na
Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TIE,Dk.Paul Mushi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa TEA na TIE mara
baada ya kumalizika makubaliano kati ya taasisi hizo iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA
ya Elimu Tanzania (TEA) imeingia makubaliano na Taasisi ya Elimu
Tanzania (TIE) ya mkopo wa sh.Bilioni Tatu kwa ajili ya kuiwezesha TIE
kufanya utafiti wa kubaini mahitaji ya mabaoresho kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali wa elimu.
Katika
utafiti huo TIE itaandaa mitaala na mihtasari ya masomo ya shule ya
msingi, kuandika vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la Sita ikiwa
ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kuingia makubaliano hayo, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TEA,Joel Laurent mkataba wa mkopo huo ni nafuu
ambao unatakiwa kulipwa katika kipindi cha miaka sita.
Amesema
TEA itaendelea kushirikiana na TIE kwa kuzingatia sera mpya ya elimu ya
mwaka 2014 na TIE kuridhia mkopo maombo ya mkopo ili kuhakikisha uwepo
mihtasari ,Mitaala na vitabu vya kiada kwa darasa la tatu hadi la sita
vinavyoendana na mahitaji.
Kwa
upande Mkurugenzi Mkuu wa TIE, Dk.Paul Mushi amesema matokeo tarajiwa
kutokana na mkopo huo ni pamoja na uwepo wa mitaala inayoendana nan a
wakati na inayokidhi mahitaji ya sekta shirikishi ,uwepo wa mihutasari
ya masomo itakayosambazwa katika kila shule kama ilivyoainishwa katika
mitaala na uwepo wa vitabu vya kiada kulingana na mitaala ili kuepusha
kuwa na vitabu vinavyotaofautiana.
Aidha amesema ufadhili unalenga kuiongezea TIE kuelekeza majukumu yake kwa njia yenye tija na kuongeza mapato ya taasisi hiyo.