Sep 30, 2015

TASOI YAZINDUA KAMPENI YA SARATANI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO BILA MALIPO YOYOTE

Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia technolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo jijini Dar.
Mshauri kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Dominista Kombe ambaye akitoa takwimu ya wagonjwa wanaofika kutibiwa katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage  akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road leo.
 Waandishi wa habari wakiendelea kuchuka habari.
 Mkutano ukiendelea

Na Michael Maurus, Dar es Salaam
ASASI isiyo ya kiserikali ya Tanzania Social Outreach Initiative (TASOI), imezindua kampeni rasmi mpango mkakati endelevu wa kuendesha kampeni ya Mshikamano dhidi ya Saratani kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano bila malipo yoyote.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TASOI, Belinda Mlingo, alisema kuwa kampeni hiyo itatoa elimu, uhamasishaji na kutoa ushauri nasaha kwa wananchi kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Amesema kuwa katika kampeni hiyo, TASOI inashirikiana na wadau mbalimbali katika masuala ya afya, teknolojia na uhamasishaji wa jamii ili kutoa huduma hii muhimu bila malipo au gharama yoyote kwa watumiaji wa simu za mikononi.
“Kwa kumnukuu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Yasiyoambukiza Wizara ya Afya, Profesa Ayoub Mgimba, ‘Hali halisi inadhihirisha kwamba magonjwa yasiyoambukiza kama saratani hivi sasa yamekuwa ni tatizo kubwa hasa katika nchi kama yetu ambapo ufahamu na mwamko ni mdogo sana juu mazingira hatarishi, viashiria, matibabu na matunzo ya wahanga wa magonjwa haya. Saratani inasababisha madhara makubwa ambayo yanaelekea kuwa majanga kwa jamii na kiuchumi kwa Taifa.”