Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Singida, Sosthenes Masolla (aliyesimama),
akifungua semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za
utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao. Semina hiyo ilifanyika mjini Singida
Septemba 5, mwaka huu. Wengine pichani ni wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na
Madini. Kutoka kushoto ni Placid Kabyemera, Juma Masoud, Mhandisi Nuru Shabani,
Mhandisi Gabriel Senge na Tantao Tantao.
Sehemu
ya washiriki wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa
leseni kwa njia ya mtandao iliyofanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu.
Semina hiyo ni mwendelezo wa zoezi la utoaji mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa
madini nchi nzima kuhusu matumizi ya huduma hiyo mpya.
Mhandisi
Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nuru Shabani, akiwasilisha mada
mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini
kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa
Wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika Septemba 5,
mwaka huu mjini Singida.
Washiriki
mbalimbali wa semina kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji wa
leseni kwa njia ya mtandao, wakiuliza maswali wakati wa semina hiyo. Semina
ilifanyika mjini Singida Septemba 5, mwaka huu.