Mgombea urais wa Tanzania kwa
tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Dodoma
kwenye mkutano wake wa kampeni.
Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John pombe Magufuli leo akiwa katika Mkoa
wa Dodoma ambao ni wa 18 kufanya kampeni zake, amefanya mikutano katika
vijiji na majimbo mbalimbali.
miongoni mwa vijiji hivyo ni Mbande,
Chunyu, Mpwapwa, Kongwa, Kibaigwa, Chalinze, Njia Panda ya Chamwino na
kumalizia na mkutano ulihudhuliwa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma.
PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKO DODOMA