Aug 30, 2015

WATEJA WA AIRTEL WAZAWADIWA MILIONI 25 KUPITIA PROMOSHENI YA JIONGEZE NA MSHIKO‏


Meneja Mauzo wa Airtel Kagera , Mohamed Kabeke (kushoto) akimkabithi pesa taslimu bwana Mwahamadi Katula (24) mfanyabiashara na mkazi wa mkoa wa Kagera , mara baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni 3 katika droo ya wiki ya tano ya promosheni ya Jiongeze na Mshiko inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Afisa uhusiano na matukio, Bi Dangio Kaniki akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya sita ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician.(kulia) droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam,.