Aug 30, 2015

VODACOM TANZANIA YASHIRIKI KONGAMANO LA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA NA UWEKEZAJI JIJINI DAR ES SALAAM‏

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutoka kushoto Anna Msinde, Mwanaidi Khaji na Mariam Rajabu wakielekezwa na Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Athuman Mwakipesile (kulia) jinsi ya kujiunga na huduma ya M-Pawa inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupata riba na mikopo ya bei nafuu kupitia simu zao za mkononi wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji(Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Athuman Mwakipesile (kushoto) akiwafafanulia jambo baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania waliofika katika banda la kampuni hiyo wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji (Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam,Idd Mawe akitoa semina ya mafunzo ya huduma ya M-pawa na M-pesa kwa Mawakala na wateja wa kampuni hiyo wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji (Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakitembelea mabanda ya Vodacom Tanzania na kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kujiunga na huduma ya M-Pawa inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupata riba na mikopo ya bei nafuu kupitia simu zao za mkononi wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji(Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.