Aug 26, 2015

TAASISI YA BILL NA MELINDA GATE YAANGALIA UWEZEKANO WA KUSAIDIA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA KILIMO NCHINI TANZANIA.

x1
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates Bw. Stanley Wood akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) nchini Tanzania kuangalia uwezekano wa taasisi hiyo kusaidia miradi ya ukusanyaji wa Takwimu za kilimo nchini Tanzania.Kushoto kwake ni Mratibu wa miradi wa Taasisi hiyo Bi.Bhramar Dey.
x2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu umuhimu wa takwimu za Kilimo nchini Tanzania na mikakati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha upatikanaji wa Takwimu za kilimo nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw.Morrice Oyuke.
x4
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof.Innocent Ngalinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya chuo anachokiongoza katika kutoa elimu kwa watakwimu wa kilimo nchini Tanzania na mpango wa chuo hicho kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za  kilimo kwa kutumia wataalam wanaozalishwa.
x5
Mtakwimu mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi.Elizabeth Talbert( kulia) na Meneja wa Idara ya Viwanda na Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Joy Sawe wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wawakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates jijini Dar es salaam.Picha na Veronica Kazimoto.