Akizungumza na paparazi wetu, Shilole
alisema kuwa adhabu aliyopewa ni kubwa mno kiasi ambacho anashindwa
kuelewa kwa kuwa sanaa ndiyo kazi inayompatia kula na hata kuwasomesha
watoto wake hivyo kumfungia mwaka mzima ni kama kumtuma kutembea hata na
waume za watu ili maisha yake yazidi kusonga mbele.
“ Mimi naona sasa wananituma kuanza
kusaka waume za watu kwa kweli kwa sababu mwaka mzima kweli na ni kazi
ambayo naitegemea kwa kila kitu katika maisha yangu kwa nini mtu
usiwaze vitu vingine kama huna kazi ya kufanya jamani, yaani inaniuma
sana,” alisema Shilole.