Jaji
Mkuu wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Roy Sarungi akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Katika ofisi za Proin
Promotions Ltd juu ya mchakato mzima wa fainali ya TMT itakayofanyika
tarehe 22 August 2015 Katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta kwa
kiingilio cha Shilingi Elfu Hamsini (50000) kwa viti maalumu na shilingi
elfu thelathini (30000) kwa viti vya Kawaida.Mshindi katika fainali
hiyo itaondoka na kitita cha Shilingi milioni hamsini (50,000,000) za
Kitanzania.
Meneja
Mradi wa Tanzania Movie Talents (TMT) Saul Mpock akiongea kuhusu jinsi
Fainali hiyo itakavyorushwa ,moja kwa moja (live) kupitia Kituo Cha
Runinga cha ITV pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii , Vilevile
amewashukuru wadau wote ambao wameweza kuipiga tafu TMT kwa mwaka huu na
kuhaidi kuendelea kukushirikiana nao kwa njia moja au nyingine.
Meneja
Bidhaa wa Paisha Godfrey Fataki ambao ndio wadhamini wakuu wa Shindano
la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 akiongelea juu ya wao kushawishika
kuamua kuidhamini Paisha mara baada ya kuona kuna umuhimu mkubwa wa
kuinua sekta ya filamu nchini huku akisisitiza Wananchi kutumia app ya
paisha katika Simu zao kwaajili ya kuweza Kujipatia bidhaa mbalimbali
kutoka kwenye makampuni mbalimbali ambayo yanapatikana ndani ya app hiyo
ya Paisha.
Fainali
ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 itafanyika mnamo
tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kuanzia saa
moja na nusu usiku huku fainali hiyo ikirushwa live kupitia kituo cha
ITV pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile blogs.
Fainali
hii itakuwa ya kipekee na ya aina yake kutokana na burudani
zitakazokuwepo na kuwafanya watazamaji kuendelea kuvutiwa kuangalia
shindano hilo mpaka mshindi atakapopatikana na kuibuka na Milioni 50 za
Kitanzania huku washiriki wa kumi waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi
bora wataweza kutengeneza filamu ya pamoja huku wakinufaika na filamu
hiyo kuanzia kutengeneza hadi kuuzwa.
Tiketi
za fainali zinapatikana Makumbusho ya Taifa Posta, Kwenye Maduka yote
ya Hussein Pamba Kali, Dar Live Mbagala, Shear Illusion Mlimani City na
Millenium Tower na Tausi Fashion Mlimani City.
Shindano
la TMT limedhaminiwa na Paisha huku wakisaidiwa na Pepsi, Camgas,
Precision Air, ITV/Radio, Global Publishers, I-View Studio, Hartman
Barbershop, Van Maria Boutique, Hussein Pamba kali, Data Vision
International