
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anna Makinda akiwa
katika Mkutano wa Kumi wa Maspika Wanawake uliofanyika kwa siku mbili
hapa Umoja wa Mataifa, Mkutano wa Maspika Wanawake, umetangulia
Mkutano wa Nne wa Maspika zaidi ya 180 unaoza leo jumatatu hapa Umoja wa
Mataifa.

Sehemu
ya Wajumbe wa Mkutano wa Kumi wa Maspika wanawake, mkutano
uliojadili mbinu za kuchagiza usawa wa kijinsia, miaka 20 baada ya
Beijing pamoja na kuhakikisha utekelezaji wa malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu Baada ya 2015.

Maspika
Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa IPU Bw. Choedhury
Saber na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong wakati wa mkutano wao
wa siku mbili uliofanyika jumamosi na jumapili, ukitangulia mkutano wa
nne wa Maspika wa Mabunge.
Na Mwandishi Maalum, New York
MKUTANO
wa Nne unaowakutanisha Maspika 180 na Manaibu Spika 35 kutoka nchi
140, unaanza leo ( jumatatu) hapa Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa.
Mkutano huu
wa siku tatu na ambao umeandaliwa na Chama cha Mabunge Duniani (
IPU), utafunguliwa na Rais wa IPU Bw. Chowdhury Saber na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Matafa, Ban Ki Moon.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu.
Mkutano
ambao Maspika wanatarajiwa kujadiliana kwa kina namna ya kukabiliana
na changamoto za Amani, Demokrasia na Maendeleo kwa maono ya Kibunge.
Mkutano
wa Nne wa Maspika, ulitanguliwa na Mkutano wa Kumi wa Maspika
wanawake, mkutano uliofanyika kwa siku mbili ( jumamosi na Jumapili).
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ann Makinda
ameshiriki kikamilifu na kuongoza baadhi ya mikutano.
chanzo: JIACHIE