Aliyewahi kuwa swahiba wa mbunge mtarajiwa Wema Sepetu, Snura Mushi ametoa kauli zenye mlengo wa kumpiga vijembe Wema.
“ Naepukana na unafiki tena naweza kusema ni roho mbaya chuki kwa
baadhi ya wasanii kuunda makundi ambayo yanatumia muda mwingi kuwadis
wengine, mfano hivi sasa wakata Diamond anawania tuzo za kimataifa eti
kuna watu wanaungana na watu wan je kufanya kampeni ashindwe,” alisema
Snura.
Snura anadai kuwa siku hizi makundi ambayo yanaundwa na wasanii au
wapenzi wenyewe ambayo yanatumika vibaya katika kutengeneza ugomvi au
kushabikia wasanii wakigombana kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwatusi
na kuwakatisha tamaa hata kama wanafanya kazi zinazotangaza Taifa.
Wema Sepetu ni miongozni mwawasanii ambao wanadaiwa kuhamasisha kundi
lake “team Wema” kumpigia chepuo msanii wa Nigeria Davido ambaye
anachuana na Diamond wa hapa nyumbani katika tuzo za MTV Africa MAMA.
KIU
