WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akirejesha fomu za wadhamini
kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajabu Luhavi, jana, baada ya
kukamilisha kazi ya kuomba udhamini kwa mikoa yote nchini.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akisaini kitabu cha wageni
ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi. Kulia ni mkewe
Faraja na kushoto ni Luhavi.
MKE
wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Faraja, akisalimiana
na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhavi ofisini kwake katika
Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati Nyalandu aliporejesha fomu zake
za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya urais.
BAADHI
ya wanachama wa CCM waliomsindikiza Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu, kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kwa
tiketi ya CCM mjini Dodoma, jana.