MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Steven Mengele ‘Steve Nyerere’
amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wana nafasi kubwa katika
uongozi kwa ni kivutio cha wapiga kura kwa mantiki ni wakati wao
kushiriki katika hatamu za uongozi, na kujiandikisha katika daftari la
mpiga kura.
"Ni kweli tunahitaji mabadiliko katika utawala lakini hilo
litafanikiwa tu pale tutaposhiriki kujiandikisha katika Daftari la mpiga
kura, kama nilivyosema badala ya kusimama badala ya mgombea sasa
tunasimama sisi tujiandikishe bila kupuuza,”anasema Steve Nyerere.
Msanii huyo mwenye kipaji cha kuigiza kuigiza sauti za viongozi
mbalimbali anasema wasanii pamoja na wananchi muda kulalamika
umechaguliwa kiongozi husiyemkubali umekwisha lazima kila mtu aache
shughuli zake kwa siku moja tu ajiandikishe katika Daftari la mpiga kura
kuwapa sapoti.
FC
