Msanii wa Bongo Fleva ambaye ameshawahi kuigiza kwenye filamu kadha
ya kupinga mauwaji ya Albino, Keisha amefunguka kupitia ukurasa wake wa
kwenye mtandao wa Instgram sababu na nia yake ya kuingia bungeni mwaka
huu,na kwamba wao kama walemavu wa ngozi (Albino) lazima wawe na
wawakilishi wa kutosha bungeni ili sauti zetu zisikike ili sheria
itungwe na kutekelezwa pia.
Kesha ameandika;
Habari za asubuhi ndugu zangu rafiki zangu mashabiki zangu na media
zote nchini.najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana juu yangu kwanini
nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na kuwaambia
kitu.
Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini
yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka
nchini kwetu.
Nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna ambao walinipongeza na
kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu kwakuwa wanahisi
nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji na
ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu.fimbo ya mbali
haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima
tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima
tuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike
ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.hivyo mimi kama mtanzania
mwenzenu nahitaji support yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa
yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi na harakati zangu anisaidie kwa
chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka.
this is my tigo no 0718785045 na hii ni account number yangu ya crdb
011 2022295800 jina ni hadija shabani Taya unaweza kuchangia humo na kwa
upendo kabisa naomba u repost hii post kadri muwezavyo ahsanteni
shukrani.
Tumuunge mkono jamani.
