
MWANASIASA
mkongwe nchini, mzee Kingunge Ngombale Mwiru, amekionya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kutofanya dhihaka ya kumpendekeza kada yoyote kuwa
mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba
mwaka huu, kwani kwa kufanya hivyo kitaanguka.

"CCM
lazima imteue mtu anayekubalika ndani na nje ya chama ili chama kiweze
kushinda, kinyume na hapo, hii ni njama ya kukifanya kishindwe kwenye
uchaguzi".
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Julai 8, 2015,
Kingunge ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na
ndani ya chama hicho alisema “ninatishwa na watu wanaotumia nguvu nyingi
kwelikweli kupambana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, badala ya
kuelekeza nguvu hizo kupambana na wapinzani wetu, hii ni hatari.’,
alionya
Amesema,
CCM ni lazima ifuate katiba yake ili wajumbe wanaotarajiwa kutoa
maamuzi watoe maamuzi sahihi na sio kupindisha katiba kwa kuanzisha
utaratibu ambao sio utamaduni wa kidemokrasia.
“kuna
kiongozi mmoja anasema, kada yeyote wa chama hicho aliyeomba kuteuliwa
kuwania urais, endapo jina lake litakatwa hatakuwa na nafasi ya kukata
rufaa, hii haijawahi kutokea na wala haipo kwenye katiba yetu.’ Amesema
Mzee Kingunge.
.Hivi
karibuni Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa hakutakuwa na
nafasi ya kada wa chama hicho atakayeenguliwa kwenye mchujo kuweza
kukata rufaa, kwani hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.
Hata
hivyo Kingunge amepinga kauli hiyo na kusema, inakwenda kinyume cha
katiba ya CCM ambayo inaweka bayana kuwa maamuzi ya vikao vya chini
yanaweza kukataliwa na vikao vya juu ikiwa ni pamoja na mwanachama
ambaye anaona hakutendewa haki kuwa na nafasi ya kupinga uamuzi wa vikao
vya chini.
na MICHUZI BLOG