
Mkuu
wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Bi. Agnes Kaganda (wa kwanza
kushoto) sambamba na mmoja wa maofisa wa benki hiyo wakitoa maelezo
kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki hiyo kwa mteja (aliyebeba
mtoto) aliyetembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viwanja vya
maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam-Saba saba mwishoni
mwa juma lililopita.

Baadhi
ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania (katikati) wakifurahia moja ya
zawadi kutoka benki hiyo walipotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo
lililopo kwenye viwanja vya maonyesho ya Biashara ya kimataifa ya Dar
es Salaam –Sabasaba. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo Mkuu
wa Matawi ya Benki hiyo Bi. Elizabeth Mayengoh (wa kwanza kushoto).
Benki ya Exim yajivunia mafaniko maonyesho ya Saba saba.
USHIRIKI
wa benki ya Exim kwenye maonyesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba
yanayoendelea jijini Dar es Salaam umeonyesha mafanikio makubwa ambapo
pamoja na fursa nyingine benki hiyo pia imefanikiwa kusogeza huduma zake
karibu kwa wateja wake wanaoshiriki na kuhudhuria maonyesho hayo.
Mbali
na kutoa ushauri wa kibenki kwa washiriki na wateja wanaotembelea banda
la maonyesho ya benki hiyo, benki hiyo pia imeweka mashine ya ATM
inayotembea jirani na banda hilo ili kuwapunguzia hadha ya kubeba kiasi
kikubwa cha fedha wateja wake wanaofanya manunuzi kwenye maonyesho hayo
sambamba na kujali usalama wa pesa zao.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye maonyesho hayo mwishoni mwa juma
lililopita, Mkuu wa Matawi ya Benki hiyo, Bi. Agnes Kaganda alisema
mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na huduma nzuri
zinazotolewa kwa weledi wa hali ya juu na maofisa wa benki hiyo
wanaohakikisha kila mteja anaetembelea banda hilo anaondoka na uelewa
wa kutosha kuhusu huduma na bidhaa za benki hiyo.
“Tumekuwa
tukipokea wateja na wageni wengi sana wanaohitaji maelezo ya huduma
zetu mbalimbali na kwa kweli pia tumefanikiwa kupata wateja wengi ambao
wamefungua akaunti zao…kifupi washiriki wengi wameonyesha kuridhishwa na
huduma zetu,’’ alibainisha.
Kwa
mujibu wa Bi. Kaganda mbali na huduma nyingine wateja wengi
waliotembelea banda la benki hiyo wamekuwa wakipewa maelezo ya kutosha
na faida kuhusu matumizi na usalama wa kadi za kutolea fedha za FAIDA
zinazotolewa na benki hiyo.
“Pia
tumekuwa tukiwahamasisha wateja na washiriki wanaotutembelea hapa
kuhusu umuhimu wa wao kufungua akaunti ya amana (fixed deposit
account)ambapo kwa sasa tunaendelea na kampeni ya kuhamasisha watanzania
kujenga utamaduni kuweka akiba,’’ alibainisha Bi. Kaganda.
chanzo JIACHIE