
Meneja
Bidhaa wa benki ya Exim, Bw Aloyse Maro akiokota moja ya kura za wateja
wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya
malengo inayoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.Wanaoshuhudia ni pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Humudi Abdulhussein (kushoto) na mmoja wa maafisa wa beki hiyo Bw George Musetti.
Benki
ya Exim Tanzania imeendesha droo yake ya kwanza ya kampeni ya akaunti
ya malengo inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa
watanzania.
Droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini iliendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ikiwa ni droo ya kwanza kati ya sita zinazotarajiwa kuendeshwa katika kampeni hiyo.
Akizungumza
mara tu baada ya droo hiyo, Meneja bidhaa wa benki hiyo, Bw. Aloyse
Maro alisema kampeni hiyo ilizinduliwa ikiwa ni sehemu ya jitahada za
benki hiyo kuwapatia wateja wake faida zaidi sambamba na huduma bora.
Alisema
kwa kuanzia, washindi waliopatakina kupitia droo hiyo walifanikiwa
kujitwalia zawadi za simu za kisasa aina ya iPhone 6 huku akitoa wito
zaidi kwa wateja wa benki hiyo kuwa na mwitikio zaidi kwa kushiriki
kwenye kampeni hiyo.
“Pamoja
na kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu kutokana na mafanikio
tunayoendelea kuyapata ni vema pia tuwe mrejesho wa mafanikio haya kwao
pia. Ni katika mazingira hayo ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kutoa
zawadi kwa wateja wetu ili kufurahi nao pamoja,’’ alisema Bw. Maro.
Zaidi
Bw. Maro aliwakumbusha wateja wa benki kuendelea kushiriki zaidi kwenye
kampeni hiyo kwa kuwa bado wananafasi zaidi ya kujishindia zawadi
mbalimbali ikiwemo zawadi ya gari kwenye droo tano zilizosalia.
“Kampeni
hii inaendelea kwa kipindi cha miezi mitano na bado kuna zawadi zaidi
kwa ajili ya washiriki ikiwemo zawadi kuu ya gari ambayo itakabidhiwa
kwa mshindi mwishoni mwa kampeni hii. Hivyo tunaomba watu waendelee
kushiriki zaidi,’’ alisema.
Sambamba
na zawadi hizo Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo inatoa riba nzuri
zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.
na JIACHIE