Katika kijiji cha Mabanda wilaya ya
Misungwi mkoani Mwanza, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania
imemuwezesha mkulima mdogo Innocent Kipondya, anayeendesha kilimo cha
mbogamboga kwa kumkabidhi zana bora za Kilimo kwa ajili ya kuendeleza
biashara yake.
Innocent alimaliza elimu ya sekondari,
kidato cha nne mnamo mwaka 2011, hakufaulu kuendelea na masomo ,
alitamania sana kufanyabiashara ya Kilimo lakina hakuwa na mtaji,
alifikiri kwenda mjini kutafuta kazi lakini hakujua pa kuanzia ndipo
alipoamua kujikita kwenye kilimo cha biashara kijijini kwao.
Airtel Kupitia mradi wake wa Airtel Fursa,
uliona juhudi za kijana Innocent za kutaka kujikomboa na maisha na
kuepukana na vishawishi vinavyowakumba vijana wengi hapa nchini hivyo
kuamua kumkabidhi zana zilizobora zitakazomuinua katiaka biashara yake.
Wakati wa makabidhiano ya vifaa vya hivyo,
Meneja wa Airtel wa huduma kwa jamii, Hawa Bayumi, alisema “leo hii
tunamkabidhi Innocent vifaa hivi kutokana na changamoto anazokumbana
nazo katika kuendeleza biashara yake. Airtel, kupitia mradi wake wa
Airtel Fursa tumeona ni muhumu kumuwezesha ili aweze kukuza biashara
yake na kuongeza thamani kwenye mazao yake na kuyauza kwa bei nzuri”.
Hawa aliongeza kwa kusema, “Airtel Fursa ni
mradi wa kijamii wenye lengo la kuhamasisha vijana, kuwapa fursa ya
kujiendeleza kibiashara na kuwapa ujuzi utakoawawezesha kuimarisha
biashara zao . Mradi huu unalenga kuwasaidia vijana wenye umri kati ya
miaka 18-24 waweze kujikwamua kiuchumi na unalenga kuwasaidia wale
vijana wanaoonyesha kujituma kiuchumi.
“Na huo sio mwisho wetu kwani Airtel Fursa
bado inaendelea kuwawezesha vijana hapa nchini. Airtel inaona fahari
kuwa sehemu ya jamii katika kuisaidia serikali kuwakwamua vijana
kiuchumi”.
Kwa upande wake Innocent aliwawashukuru
Airtel kwa kusema, “nawashukuru sana Airtel kwani wameweza kubadili
maisha yangu na familia yangu. Kwani kutokana na zana duni kwa wakulima
wa mbogamboga vijijini ni aina nyingine ya vikwazo vinavyotukwamisha
wakulima tusifikie malengo ya kupanua kilimo na kupata mazao mengi
mashambani”.
“Mbali na zana duni, baadhi ya wakulima
vijijini wanalima bila kufuata kanuni bora za kilimo na hivyo kujikuta
tukipata mazao hafifu. Kutokana na elimu niliyopewa na Airtel ninaamini
kabisa nitaweza kuboresha biashara yangu na kuwa mfanya biashara mkubwa
hapa nchi na hata nje ya nchi.”
“Ili kijana kama mimi aweze kufaidika au
kushiriki kwenye Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa
namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara
na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe
airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na
aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia
yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com