| Rais Dr Jakaya Kikwete akipata maelezo ya bidhaa za Asas Daireis Ltd kutoka kwa afisa masoko wa kampuni hiyo Bw Jimy alipotembelea mabanda mbali mbali katika maonyesho ya sikukuu ya sabasaba yanayotaraji kuhitimishwa kesho jijini Dar es salaam |
| Rais Dr Kikwete akipata maelezo ya bidhaa za Asas Daireis Ltd kampuni hii ni ndio kampuni bora ya usindikaji maziwa nchini Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo sasa |
| Rais Dr Kikwete akitazama baadhi ya bidhaa zenye ubora za kampuni ya Asas Daireis Ltd |
| Rais Dr Kikwete akifurahia baada ya kutembelea banda ya Asas DaireisLtd jijini Dar es Salaam |
| Wananchi mbali mbali wakitembelea banda ya Maziwa ya Asas katika viwanja wa Sabasaba jijini Dar es Salaam |
Na MatukiodaimaBlog
BANDA
la kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya mkoani
Iringa lililopo limeendelea kuwavuta wananchi na viongozi mbali
mbali wanaotembelea viwanja wa Saba saba jijini Dar e Salaam
kulitembelea kupata bidhaa zake
Banda
hilo ambalo wiki iliyopita lilitembelewa na Rais Dr Jakaya
Kikwete na viongozio mbali mbali limeendelea kuvutia wananchi
wengi wanaotembelea maonyesho hayo kupenda kufika kupata bidhaa
mbali mbali .
Baadhi
ya wananchi waliofika katika banda hilo walisema kuwa
wamevutiwa zaidi ya bidhaa zenye ubora zinazotengenezwa na kampuni
hiyo ya Asas Dairies Ltd kutoka mkoani Iringa na hivyo kulazimika
kumiminika zaidi kupata bidhaa pamoja na kupata elimu mbali mbali
ya ubora wa bidhaa hizo .
Alisema
Amina Athuman ambae ni mmoja wa wateja waliofika katika banda
hilo kupata bidhaa mbali mbali , kuwa yapo makampuni mengi ya maziwa
ila ubora wa bidhaa za maziwa zinazotengenezwa na kampuni hiyo ya
Asas Dairies Ltd ndizo ambazo zinawavutia watu wengi zaidi kufika
katika banda hilo.
"
Mimi nilikuwa nasikia tu juu ya ubora wa maziwa haya toka mkoani
Iringa ila baada ya kufika hapa nimeshuhudia na kuanzia leo
sihitaji maziwa na bidhaa nyingine kama hizi nje ya Asas Dairies Ltd
"
Huku
John Mwene akieleza kufurahishwa zaidi na hatua ya Rais wa nchi
Dr Kikwete kutembelea mabanda ya wakulima mbali mbali likiwemo
banda hilo la Asas kwani ni ukweli usiopingika kuwa kwa Tanzania
kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd imeonyesha uwezo mkubwa wa kuzifanya bidhaa zake kuendelea kuwa na ubora kwa miaka mitatu mfululizo.
Kwani
alisema kampuni kuongoza miaka mitatu mfululizo ni jambo la
kujipongeza na kuwa si rahisi kwa kampuni kushikilia ubora wake kwa
miaka miwili mfulilizo ila kampuni hiyo imeweza kufanya hivyo .
Alisema
ni jambo la nchi kupitia bodi ya maziwa na wizara husika kuangalia
kutoa uwezeshaji zaidi kwa makampuni bora ili kuwezesha bidhaa zake
kuingizwa katika soko la dunia .
Afisa
masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Bw Jimmy
Kiwelu pamoja na kumpongeza Rais Dr Kikwete kwa kutembelea banda lao
na kupongeza kwa ushiriki na ubora wa bidhaa zao bado aliwashukuru
wananchi wanaoendelea kutembelea banda hilo .
Alisema
kuwa mbali ya kampuni hiyo kuonyesha ushiriki mzuri katika maonyesho
hayo ya saba saba bado wamekuwa wakishiriki maonyesho mbali mbali
yakiwemo yale ya nane nane kwa kushiriki katika kanda mbali mbali na
kuwataka wananchi wa kanda zote nchini kujipanga kwa ajili ya
kutembelea mabanda yao wakati wa nane nane mwaka huu .
Kuhusu
kuendelea kuongoza kwa ubora alisema kuwa hivi sasa ni mwaka wa
tatu mfululizo bado bidhaa zao nyingine zimeendelea kushinda
medali mbali mbali na kuonyesha uwezo mkubwa wa kampuni hiyo katika
ubora .
HABA NA JIACHIE