Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye ametangaza nia kuwania
ubunge wa Viti Maalum kupitia CCM ameandika hayo kwenye ukursa wake
Instagram mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu ya zamani akiwa na
mama yake pamoja na Marehemu baba yake.
"Naanza kwa kusema Alhamdulillah kwa kufikia hapa nilipo
na nawashkuru sana wazazi wangu kwa kunileta duniani na kunilea katika
maadili mazuri.
Nawashkuru pia kwa kunipa Elimu na kunipa chochote
nilichokitaka but more over kwa kunipa support kubwa katika uamuzi
wowote niliokuwa nimeufanya. Kwanzia kushiriki Miss Tanzania mpaka pale
nilipoamua kujiingiza katika maswala ya sanaa.
Vitabu vya dini vimeandika inapaswa tumshukuru Mungu kwa
kila jambo, liwe zuri au baya... Pale Mungu alipoamua kumchukua Daddy
Sepetu wangu niliumia sana na nikawa nimeona kama maisha yangu yalirudi
nyuma kidogo, maana ilinibidi nianze kuishi maisha ya No More Daddy
Sepetu.
Maana nilikuwaga ni kipenzi cha Daddy wangu cuz I happen
to be da last born, mwenyewe alikuwa akiniita Miss World wake....
Nakumbukaga My Late Daddy Sepetu alishawahi kuniambia kuwa nijaribu
kujiingiza katika politics since yeye na siasa ilikuwa ni kama uji na
mgonjwa... And I remember nilimwambia ,"Daddy Sepetu NO sitoweza" ...
Alikuwa heart broken sana maana alihisi nikijaribu ntaweza na
kilichokuja kumvunja moyo ni nilipochukua uamuzi wa kufanya
International Business na sio hata Political science au chochote
kilichohusu Siasa nilipoenda Chuo... But hakukata tamaa... Akazidi
kuniambia naweza na nilizidi kukataa... Daddy Sepetu wangu This is for
u....
Leo hii nimejikuta mwenyewe nimefanya uamuzi mzito wa
kujiingiza kwenye Siasa na kuona wat it has in store for me... Najua you
are looking down on me smiling... Ila tu jua kuwa Your wife ambaye ni
my Darling Mother nae pia amechangia kiasi kikubwa sana... Nawapenda
sana wazazi wangu maana wanajua Whats Best for me... Haya sasa naingia
vitani... Na sitokubali Defeat... Tho kuna mengi yanaweza tokea...
Namkabidhi Allah yote.... Na niko tayari kwa chochote...
Penye nia siku zote njia haiwezi kukosekana..."-Wema ameandika
Kila la kheri Madam
chnazo: bongomovies
