Walimu ambao walilitoroka eneo la
kazkazini mashariki mwa Kenya wakihofia mashambulizi kutoka kwa kundi la
wapiganaji wa Al shabaab wamekataa kurudi eneo hilo.
Mwandishi wa
BBC Bashkas Jugsodaay alielezea katika kipindi cha Newsday kwamba
asilimia 60 ya walimu hawatoki katika eneo hilo na waliokwenda likizo
wengi wamekataa kurudi.Ameelezea kuwa takriban walimu 2000 wamelitoroka eneo hilo na kwamba nusu ya idadi ya shule za eneo hilo zimefungwa.
Amesema kuwa wafanyikazi wa uma pia wamelitoroka eneo hilo.
