
Marekani imetumia zaidi ya dola
bilioni mbili unusu katika kufadhili vita dhidi ya Islamic State,
kupitia kutekeleza mashambulizi ya angani nchini Iraq na Syria tangu
mwezi Agosti mwaka jana.
Makao makuu ya Pentagon yametoa orodha ya
gharama ya fedha zilizotumika, inayoonyesha kuwa inatumia zaidi ya dola
milioni tisa kwa siku katika kutekeleza operesheni hiyo.Bunge la Marekani limekataa jaribio la kuzuia matumizi zaidi ya fedha ili kukabiliana na IS.
Bunge la wawakilishi limepitisha mswaada wa kuikubalia wizara ya ulinzi kutumia dola bilioni mia tano na themanini.
bbc