Wabunge waitaka serikali kuboresha miundombinu
Wabunge wameendelea kuchangia bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa
fedha wa 2015/2016 ambapo baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuboresha
miundombinu ikiwemo ya reli, barabara na maji.
Ikiwa ni muda wa lala salama kwa bunge la KUMI, baadhi ya wabunge wametumia sehemu ya muda wao kuaga wenzao, wengine wamechangia kwa hisia, huku wakitahadharishana katika matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu
Baadhi ya wabunge hao wamependekeza serikali ichambue Bajeti kuu kwa undani /kwa kulinganisha na mwaka uliotangulia ili iweze kuwa na tija miongoni mwa Watanzania.
Baada ya majadiliano haya, Mawaziri wenye dhamana watapata nafasi ya kutoa majawabu /hoja maombi na ushauri wa wabunge.
TBC
