Afisi ya juu katika serikali ya Uingereza imeiambia BBC kuwa ililazimu
majasusi wa Uingereza kuhamishwa kutokana na sababu kuwa Urusi na China
zifanikiwa kupata taarifa za kisiri jinsi zinavyoendesha shughuli zake
zilizoibiwa na jasusi raia wa marekani Edward Snowden.
Gazeti la Uingereza la Sunday Times linasema kuwa Urusi na China
walidukua nyaraka kwenye mitandao. Serikali ya Uingereza inasema kuwa
hakuna dalili kuwa udukuzi huo umesababaisha madhara yoyote.
Edward
Snowden ambaye ni mwanakandarasi wa zamani katika shirika la ujasusi la
marekani , aligonga vichwa vya habari miaka miwili iliyopita baada ya
kifichua ujasusi wa mitandao na wa simu uliokuwa ukiendeshwa na Marekani
na Uingereza. Kwa sasa anaishi nchini Urusi.
BBCSWAHILI.COM

